TICO EDITOR

Thursday, May 19, 2011

OMARY CLAYTON KUJADILIWA NA MASTAA WAKUBWA

Msanii OMARY CLAYTON  kijana alieanza sanaa ya maigizo tangu akiwa na umri mdogo sana katika kikundi cha Kaole sanaa group nyota yake ilianza kung'ara pale alipoteuliwa katika wasanii walioshiriki katika tamthilia ya FUNIKO vilevile akiwa bado yupo kaole akachaguliwa kushiriki tamthilia ya TETEMO,Omary alionyesha uwezo mkubwa sana kiasi cha kuzikonga nyoyo za watanzania wengi na kujizolea mashabiki rukuki ndani na nje ya Tanzania,baada ya hapo alijiunga mojakwamoja na uigizaji wa firamu na kupata nafasi ya kucheza firamu ya WICKED LOVE ya msanii Vicent Kigosi akiwa ndani ya uigizaji akapata ujuzi wa uandishi wa story za movie ambapo alianza na story SHAKIRA ambayo ilichezwa na Vicent Kigosi pamoja na Iren Uwoya,baada ya hapo Omary aliandika story ya movie iitwayo HEKIMA na kuicheza mwenyewe akishirikiana na wasanii kama Hemedi Suleimani,Wastara Juma,Juma Kilowoko movie ambayo imefanya vizuri sana katika soko la filamu Tanzania kiasi cha kuwafanya mastaa wakubwa kukaa vikao vya kujadili kuhusu mapinduzi aliyoyafanya msanii OMARY CLAYTON ambaye kwasasa anapatikana katika filamu ya HOME VILLAGE ambayo pia imeongeza mjadala mkubwa katika tasnia ya filamu Tanzania,msanii Omary amesema kuwa yeye kwa sasa amejiunga na kampuni ya TIMAMU EFFECTS kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika tasnia ya filamu na kuwa yuko tayari kupambana na wote wanaotaka kumrudisha nyuma pia amewataka wadau wa filamu nje na ndani ya Tanzania kukaa tayari kuipokea HOME VILLAGE.