TICO EDITOR

Friday, February 25, 2011

HOME VILLAGE SASA IPO JIKONI

 Hapa kazi ikiendelea
 Denis David naye amepata nafasi yakuonyesha kipai chke
 Mi nawaita maembe  ya TIMAMU EFFECTS Jackson na Denis
 Hili ni zao jipya  katika tasnia ya filam anaitwa ANGEL naye ameonyesha ujuzi ndani ya HOME VILLAGE
Bashiri production designer wetu naye ameshiriki
Mwanadada ANGEL yupo kazini
Badra akiwa katika moja ya scene za filam hiyo
The Best cameraman in TZ TIMOTH CONRAD au wengi wanapenda kumuita TICO akiwa kazini
Yani full mauaji ndani ya HOME VILAGE
kazi kama kawa
Rashid mrutu naye alikuwepo location kutoa 'sapoti'
hapa baada ya kutoka kupiga scene moja ngumu sana
JEMBEEE anaitwa HAMISI CHECHE wakazi wa mabibo wanamfahamu maana ndiye mtemi wao naye ameshiriki katika filam hii
TICO TICOLA KAMA KAWA
Moja ya scene ngumu alizocheza bashiri bashirima
duu jack kwa kujituma tuu hajambo
JEMBEEE wanamuita 50 cent sijui kwanini lakini naye ameshiriki
hapa tuko pamoja 
full shangwe ikifika jioni tukiwa kambini kwetu kwa mzee joto
 Usister duu kando hapa kazi kwanza
duu ebwana tulichoka kinoma

Friday, February 4, 2011

FILAMU MPYA YA 077 DAYS NUSURA IMTENGUE KIUNO SAJUKI

JUMA KILOWOKO (SAJUKI) AKIUGULIA BAADA YA KUUMIA WAKATI WA UTENGENEZAJI WA FILAMU YA 077 DAYS
 HAPA AKIPATIWA HUDUMA YA KWANZA
 AKIJARIBU KUNYANYUKA 
HAPA AKITABASAMU MARA BAADA YA KUPATA NAFUU



TIMAMU EFFECTS KUTOA ZAWADI KWA WADAU

Kampuni ya utengenezaji wa filamu nchini Tanzania TIMAMU EFFECTS chini ya uongozi wa TIMOTH CONRAD (TICO) editor aliyewafanya baadhi ya ma-editor wa filam za kitanzania kurudi shule baada ya kugundua kuwa kuna baadhi ya vitu bado hawajavijua ambavyo wamekuwa wakiviona katika kazi ambazo zimefanywa na TICO akiwa ndani ya kampuni hiyo ya TIMAMU EFFECTS.

Bila shaka jina la filamu kama VITA ambayo imewakutanisha wasanii maarufu kama vile juma kilowoko{sajuki}wastara,mwisho mwampamba ambaye alikuwa ni mshiriki wa BBA{big brother africa}denis sweya{dino}na wengine wengi hiyo ni moja wapo ya kazi zilizofanyika katika kampuni hiyo,vilelevile kuna kazi kama MY NEPHEW filamu ambayo imetikisa sana soko la filamu ndani na nnje ya tanzania pia imekutanisha wasanii mahiri kama jackson kabiligi{bob jack} doki,na wasanii kutoka nnchini botswana na south africa ambako ndiko ilipochezewa filamu hiyo,pia kuna filamu inayokwenda kwa jina la THE KILLER ambayo ilipokelewa kwa mikono yote miwili sokoni,kiukweli mpaka sasa ukitamka neno TIMAMU EFFECTS bila shaka kwa wale wadau na wapenzi wa filamu tanzania na nje ya tanzania moja kwa moja wanaelewa unaongelea kampuni ambayo inafanya kazi katika ubora wa kimataifa na utakumbuka kazi kama ,DAMALISA,na BRIFCASE.

Kampuni hiyo ambayo kwasasa ipo mbioni kuachia filamu kazaa ambazo ziko tayari na baadhi zikiwa mbioni kukamilika kazi hizo ni pamoja na RED & GREEN,THE SKENDO,HOME VILLAGE ni filamu ambazo zinatarajiwa kuleta mapinduzi ya ukweli katika tasnia hii ya filamu tanzania.


Director, editor na cameraman TIMOTH CONRAD baada ya kupokea pongezi kutoka kwa wadau na wapenzi wa filamu tanzani yeye pamoja na crew nzima ya kampuni ya TIMAMU EFFECTS wameamua kutoa special thanx kwa wadau na wapenda filamu za kutisha hapa nchini kwa kuandaa filamu mpya ya kutisha itakayoitwa HOME VILLAGE,
kwa sasa crew nzima ipo location katika kuikamilisha filamu hiyo ya aina yake na ambayo haijawahi kutokea bongo...