TICO EDITOR

Friday, February 4, 2011

TIMAMU EFFECTS KUTOA ZAWADI KWA WADAU

Kampuni ya utengenezaji wa filamu nchini Tanzania TIMAMU EFFECTS chini ya uongozi wa TIMOTH CONRAD (TICO) editor aliyewafanya baadhi ya ma-editor wa filam za kitanzania kurudi shule baada ya kugundua kuwa kuna baadhi ya vitu bado hawajavijua ambavyo wamekuwa wakiviona katika kazi ambazo zimefanywa na TICO akiwa ndani ya kampuni hiyo ya TIMAMU EFFECTS.

Bila shaka jina la filamu kama VITA ambayo imewakutanisha wasanii maarufu kama vile juma kilowoko{sajuki}wastara,mwisho mwampamba ambaye alikuwa ni mshiriki wa BBA{big brother africa}denis sweya{dino}na wengine wengi hiyo ni moja wapo ya kazi zilizofanyika katika kampuni hiyo,vilelevile kuna kazi kama MY NEPHEW filamu ambayo imetikisa sana soko la filamu ndani na nnje ya tanzania pia imekutanisha wasanii mahiri kama jackson kabiligi{bob jack} doki,na wasanii kutoka nnchini botswana na south africa ambako ndiko ilipochezewa filamu hiyo,pia kuna filamu inayokwenda kwa jina la THE KILLER ambayo ilipokelewa kwa mikono yote miwili sokoni,kiukweli mpaka sasa ukitamka neno TIMAMU EFFECTS bila shaka kwa wale wadau na wapenzi wa filamu tanzania na nje ya tanzania moja kwa moja wanaelewa unaongelea kampuni ambayo inafanya kazi katika ubora wa kimataifa na utakumbuka kazi kama ,DAMALISA,na BRIFCASE.

Kampuni hiyo ambayo kwasasa ipo mbioni kuachia filamu kazaa ambazo ziko tayari na baadhi zikiwa mbioni kukamilika kazi hizo ni pamoja na RED & GREEN,THE SKENDO,HOME VILLAGE ni filamu ambazo zinatarajiwa kuleta mapinduzi ya ukweli katika tasnia hii ya filamu tanzania.


Director, editor na cameraman TIMOTH CONRAD baada ya kupokea pongezi kutoka kwa wadau na wapenzi wa filamu tanzani yeye pamoja na crew nzima ya kampuni ya TIMAMU EFFECTS wameamua kutoa special thanx kwa wadau na wapenda filamu za kutisha hapa nchini kwa kuandaa filamu mpya ya kutisha itakayoitwa HOME VILLAGE,
kwa sasa crew nzima ipo location katika kuikamilisha filamu hiyo ya aina yake na ambayo haijawahi kutokea bongo...