TICO EDITOR

Friday, March 4, 2011

HEKIMA YAMTENGUA MKONO OMARY CLAYTON

Omary clayton maarufu kama omy aliyewahi kung'aa katika drama (michezo ya luningani) kupitia kaole sanaa group, na pia aliwahi kushiriki katika baadhi ya filamu kadhaa hapa nchini kama The killers, Home Village, na nyingine nyingi ambazo bado hazijaingia kunako masoko.
     hivi karibuni nusura apate kilema cha maisha kwa kuvunjika mkono alipokuwa akicheza filam mpya itakayokwenda kwa jina la HEKIMA, iliyowashirikisha wasanii wenye uwezo katika fani ya uigizaji, sakata hilo lilitokea pale ambapo Omy alipokuwa akicheza na Hemed suleiman.
"kiukweli pamoja na kuigiza lakini nilipata kipigo cha ukweli kutoka kwa hemedi nilipocheza kama amenifuma nikiwa na mkewe (wastara), mwanzoni nilidhani kwamba hemed alikuwa anafanya kusudi lakini nilikuja kugundua kuwa ule ulikuwa ni  mzuka wa kazi hivyo sikugombana nae zaidi nilimshukuru kwa kunipa sapoti ya kutosha kupelekea mimi kucheza katika uhalisia" alisema Omary alipoulizwa baada ya kumaliza kucheza scene hiyo.
     kwa upande wake hemed alisema kuwa dogo ni muelewa ndomana hakuweza kupanik nilipomuumiza kwani anajua hizi ni kazi so haipaswi kupaniki na yeye anaelewa mizuka ya kazi ilivyo.
"lakini pia nashukuru mungu anaendelea vizuri na mkono wake umerejea katika hali yake ya kawaida niko peace na mshkaji hatuna bifu maana watu wakisikia mimi na omy tumegombana wataanza kuzusha bifu" alimalizia Hemed
katika kuthibitisha hilo hemed alipiga picha ya pamoja na Omy ili kuondoa tofauti zao.

HAPA OMARY CLAYTON AKIWA NA HEMED BAADA YA SCENE HIYO

TIMAMU EFFECTS inampa pole omy na kumwambia kuwa akaze buti ndo kazi lakini pia tunawaambia mashabiki wa filam kuwa wakae mkao wa kula kuisubiri filamu hiyo ya aina yake iliyoshirikisha wasanii kama WASTARA JUMA, HEMED SULEIMAN, JUMA KILOWOKO, MAINDA SUKA, CHARLES MAGARI, OMARY CLAYTON, pamoja na hao wakali kushiriki pia filam hiyo imeongozwa na OMARY na kupigwa picha na KABUTI ONYANGO kutoka katika kampuni ya JML PRODUCTION.