TICO EDITOR

Saturday, June 4, 2011

SANAA YA BONGO ILI IKUWE YAHITAJI KUJITUMA,DADY

Msanii DADY RAMADHANI kutoka S.A ambaye kwa sasa yuko nchini tanzania kwa ajiri ya kukamilisha baadhi ya movie,amesema kuwa sanaa ya hapa tanzania inahitaji kujituma sana ili iweze kuleta ushindani na mataifa mengine ambayo kwa sasa yamefika mbali na kuwafanya wasanii wenyewe kunufaika na kazi zao tofauti na hapa nchini msanii bado ana hali duni,DADY amesema kazi ambazo amefanya mpaka sasa moja tayari imekamilika na ipo tayari kuingia sokoni wiki hii ambayo ni filamu ya home village pia amesema kuwa filamu hiyo ataleta mabadiliko sana kutokana na jinsi ambavyo wasanii wamejituma na kufanya kitu ambacho bilashaka kitaleta mabadiliko katika tasnia hii ya filamu tanzania

Wednesday, May 25, 2011

RAMADHANI PII, UJIO WANGU NI ZAIDI YA RADI

Msanii chipukizi wa filamu Tanzania Ramadhani Pii ambaye ameshiriki katika filamu ya HOME VILLAGE ameongea na chanzo chetu cha habari hapo jana katika viwanja vya mwalimu nyerere dar-er-salam msanii huyo akiwa anatokea inchini kenya nairobi kwa ajili ya maandalizi ya filamu ya TARAFA YA WAFU filamu hiyo itayomkutanisha na wasanii mahiri wa hapa nchini Tanzania kama Omary Clayton,Denis David,Jackson Kabirigi,Dady na wengine wengi,PII amesema kuwa amejiandaa vizuri sana kuonyesha uwezo wa kimataifa na kuwapa ratha watanzania

UMOJA WA WANA TIMAMU EFFECTS NDIO SIRAHA YAO

Kampuni maarufu ya kuandaa filamu inchini Tanzania TIMAMU EFFECTS wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kazi nzito,msemaji mkuu wa kampuni hiyo bw. Timoth Conrad amesema kuwa umoja na ushirikiano walionao ndio moja ya siraha yao katika utendaji wakazi na kuongeza kuwa wamewaandalia watanzania kazi ambayo itakuwa ni utambulisho wa ujio mpya kabisa tofauti na kazi ambazo wamezifanya awali,ni filamu iitwayo HOME VILLAGE ambayo ipo katika hatua za mwisho kuingia sokoni,amemaliza kwa kuwashukuru watanzania kwa ushirikiano ambao wanauonyesha na kuwaomba waendelee kuwa makini katika kuangalia kazi ambazo zinafaa zenye mafundisho na zenye kuzingatia maadili.

DADY RAMADHANI BACK FROM JO'BURG CITY TO HOME VILLAGE

Msani maarufu DADY RAMADHANI kutoka S.AFRICA na kwasasa yupo inchi Tanzania kwa ajiri ya kushiriki katika filamu ya HOME VILAGE ambayo meshirikiana na wasanii mahili wa hapa inchini Tanzania akiwemo msanii JACKSON KABIRIGI,DENIS DAVID,OMARY CLAYTON,LATIFA IDABU na wengine wengi,filamu hiyo ikiwa tayari kwa ajiri ya kuingia sokoni DADY amesema kuwa watanzania watarajie filamu yenye ubora wa kimataifa na kuwa ahidi kuwa kwasasa bado yupo Tanzania kwa ajili ya kufanya mapinduzi katika tasnia hii ya filamu Tanzania.

HOME VILLAGE SASA TAYARI KUINGIA SOKONI

Kwa wale wadau na wapenzi wa filamu Tanzania waliokuwa wakisubilia kwa hamu sana filamu ya HOME VILLAGE baada ya kuyaona matangazo mengi katika vyombo vya habari mbalimbali sasa ipo tayari kuingia sokoni,filamu hiyo ambayo imewakutanisha wasanii kutoka ndani na nje ya tanzania,kazi hiyo ambayo inatarajiwa kufanya vizuri na kuleta mapinduzi katika tasnia ya filamu Tanzania,
Baada ya kufanya kazi kwa nguvu lengo lilikuwa ni moja tu kufanya kazi itakayopokelewa na wapenzi wa filamu kwa mikono miwili, na kukubali kuwa watu wanafanya kazi bila kuwa na masihara, sisi yaani mimi na crew yangu ya Timamu tumekusudia kuleta mapinduzi ya vitendo na si maneno” Anasema Bob Jack

Thursday, May 19, 2011

KIUNGO KIPYA NDANI YA TIMAMU EFFECTS

IBRAHIM LUHIZO nikijana wa kitanzania mwenye umri mdogo sana ila mwenye uwezo na kipaji kikubwa katika uandaaji wa filamu ambaye kwa sasa amejiunga na kampuni kubwa nchini tanzania TIMAMU EFFECTS ikiwa ni moja ya kujiongezea uwezo na uzoefu kutoka kwa wataalamu kama TIMOTH CONRAD,editor huyo IBRA ambaye ameanza kuonyesha uwezo wake katika filamu iitwayo MUMIANI ambayo inatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni,amesema kuwa amefurahi sana kujiunga na kampuni kubwa ya TIMAMU EFFECTS anaimani atafanya kazi kwa ufanisi wa hari ya juu na kuleta mabadiliko katika soko la filamu Tanzania,na amewasii watanzania kuwa wawe waangalifu na makini katika kuchagua filamu za kuangalia na si kuchagua majina ya watu maarufu.