TICO EDITOR

Wednesday, January 26, 2011

WASTARA, SAJUKI, YUSUF MLELA, DINNO WATEMBELEA WATOTO YATIMA JIJINI MWAMZA

 HAMIDA GENIUS AKIPATA CHAKULA CHA MCHANA PAMOJA NA WATOTO YATIMA JIJINI MWANZA
 JAMAA ANAITWA SENJERE NAYEYE ALIKUWEPO KUTOA BURUDANI
 UKITAZAMA VIZURI UTAMUONA WASTARA, YUSUF MLELA NA WENGINE KATIKA PICHA YA PAMOJA
 TUCHEZE PAMOJA JAMANI SISI NIWAMOJA DEFFERENT COLOR ONE PEOPLE
 
 BAADA YA SHUGULI KUISHA
 KUSHOTO NI DINO KULIA NI YUSUF MLELA
 JUMA KILOWOKO
 TUKO PAMOJA
 MLELA NA SAJUKI
 WASTARA AKITUMBUIZA
DINO AKIMNONG'ONEZA KITU SAJUKI

Thursday, January 6, 2011

LETHAL POISON INAZIDI KUFANYA VIZURI SOKONI

filam ya lethal poison ambayo imeingia sokoni wiki moja iliyopita, inaendelea kufanya vizuri kimauzo.

"Licha ya kwamba tumepata hasara sana katika utengenezaji wa filamu hiyo, kwa sasa nafarijika kwani watanzania wameonyesha kuikubali na kuipokea kwa mikono yote miwili naamini kama wakiendelea kuinunua kwa kasi kama ilivyokuwa kwa wiki hii ya kwanza nitafarijika zaidi" alisema Jairos kachota ambaye ndiye 'producer' wa filamu hiyo.

ndani ya filam hiyo iliyorekodiwa mkoani mbeya pia ameshiriki gwiji wa filam za kitanzania steven kanumba pamoja na wasanii wengine wa mkoani mbeya akiwemo Dennis Louis, Thomas na wengine wengi.

"Filam ya lethal poison ni nzuri na kilichonifurahisha zaidi editing iliyofanyika imeifanya filamu hiyo iwe nzuri zaidi" alisema Steven Kanumba.
cameraman aliyepiga picha filamu hiyo ni Timoth conrad 'TICO' vile vile yeye ndeye aliyeifanyia editing akiwa katika kampuni ya TIMAMU EFFECTS.

MIMI NA JACK KWA SASA SIO WAPENZI - SABRINA

hivi karibuni kulikua na uvumi juu ya uhusiano baina ya wasanii wawili wafilam walioshiriki katik filam ya cross roads, Jackson Kabirigi a.k. Nunda na Sabrina.
Habari zilizotufikia kutoka kwa chanzo chetu cha habari zilisema kuwa wasanii hao wawili wamekuwa wakionekana katika kumbi mbalimbali wakiwa pamoja katika mikao isiyoeleweka ( '0' distance ) chanzo chetu cha habali kilipeleleza na kupata kuzungumza na rafiki wa karibu wa jackson ambaye hakupenda jina lake liandikwe alisema
"kwakeli jack aliwahi kuniambia kuwa kuna mmoja kati ya wasanii alioshiriki nao katika filam yake mpya ya cross road kuwa "anakula mzigo" lakini hakuwahi kuniambia ni nani, hivyo hata mimi nashangazwa nakitendo cha yeye kuwa karibu sana na sabrina mi nahisi kuna kitu kinaendelea between them"

Timamu habari haikuchoka ikamtafuta jack mwenyewe ili aeleze ukweli juu ya hili lakini hakuweza kutoa ushirikiano wakutosha juu ya hilo
"siko tayari kulizungumzia hilo swala kwa sasa labda uniulize ninatarajia kutoa filam gani kwa sasa na sio huo u***" alimalizia jackson na kukata simu

Pamoja na hayo hatukukata tamaa tukatia maguu mpaka nyumbani kwa sabrina
"si mara ya kwanza kuulizwa swali hilo na sijui ni kwanini watu wanapenda kufatilia mambo ya watu, ki ukweli kabisa mimi na jack hatuna uhusiano wa kimapenzi bali ni marafiki tu nawashangaa wanaodhani mimi na jack ni wapenzi" alisema sabrina kwa msisitizo pia alipoulizwa kuwa kwa sasa anatoka na nani alisema "ninae mtu ninaempenda kwa sasa lakini siko tayari kumuweka wazi ila muda utakapofika nitaweka wazi kila kitu" alimalizia sabrina.

DOCTOR SLAA APATA KIPIGO AKIWA KATIKA MAANDAMANO YA AMANI JIJINI ARUSHA





MABOMU, RISASI, VIPIGO na hatua ya Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana vilisababisha amani kuvunjika na damu kumwagika katika mitaa ya jiji la Arusha wakati jeshi hilo likijaribu kuwasambaratisha maelfu ya wafuasi waliokuwa katika maandamano ya amani.

Wednesday, January 5, 2011

TINO MWIZI - PRODUCER AKIM

Muandaaji wa filam nchi Tanzania Akim Natibu maarufu kama Akim Producer, aliyewahi kuandaa filam ya damalisa, ameieleza Timamu Habari juu ya kitendo cha kihuni alichofanyiwa na Msanii wa filam nchini Tanzania Hisani Hassan Muya maarufu kama Tino.

"mwanzoni nilimwamini sana na nilitamani kumpashavu ili awe mmoja kati ya washiriki katika filam yangu mpya ninayoiandaa hivi sasa, hivyo tukafikia makubaliano ya bei na akahitaji nimlipe advance (kianzio) ili itakapofika siku ya kuanza kazi ya kurekodi filamu hiyo nimalizie kiasi kilichobakia, lakini cha kushangaza siku mbili kabla ya kazi kuanza nilimpigia simu ili kumkumbusha juu ya kazi hiyo alinambia kuwa yupo zanzibar kikazi na siku hiyo itakapofika atakuwa amesharudi hivyo ataweza kufika location" alisema Akim Producer

pia aliendelea kusema kuwa chakushangaza ilipofika siku ya kazi Tino hakutokea location na alipopigiwa simu hakupokea hivyo ikabidi achukuliwe mtu mwingine ili awezekukava nafasi yake, lakini baada ya siku mbili tangu kazi ianze akim alimpigia tena simu na safari hii alipokea na kusema kuwa bado hajarudi na siku atakaporudi atarudisha pesa aliyopewa kama advance kwani kazi yenyewe hakuifanya.

"lakini chakushangaza nimepata habari kuwa tayari amekwisharudi na yupo hapa dar na nikimpigia simu ili nionane nae anipatie hela yangu amekuwa hapokei simu yangu" alisema akim kwa uchungu wakuibiwa pesa zake.

kadhalka pamoja na kumdhulumu pesa pia akim amesema kuwa amemdhulumu pia jina la filamu hiyo ( HARD TIME ).

"wakati namkabidhi script ya filam yangu ya hard time tino aliwahi kuniambia kuwa anataka nimuuzie jina hilo kwani amelipenda lakini sikumkubalia matokeo yake hivi juzi niliona tangazo la filam mpya ambayo yeye tino pia ameshiriki ikiwa inaitwa HARD TIME kama jinsi jina la filam yangu ilivyo" alisema akim

"kwakeli Bado sijamsamehe Tino kwakitendo alichokifanya ila ninachokitaka anilipe pesa zangu na kuhusu swala la jina la filam sina wasi wasi kwani ninajiamini kuwa ninauwezo mkubwa katika utunzi wa filam hivyo nitaweza kupata jina lingine" alisema akim

Timamu Habari baada ya kupata habari hizo ilimtafuta Tinno ili kumuuliza juu ya tuhuma hizo bila mafanikio kwani hakupokea simu... lakini tunachoweza kukisema kama maneno ya Akim Producer niyakweli basi Tino inampasa arudishe pesa za watu ili asijichafulie jina na si vizuri kufanya kitendo kama hicho.

Monday, January 3, 2011

EID PALMER ON "A MOMENT WITH" IS COMING SOON

Eid Palmer mtangazaji wa kipindi kipya kabisa cha A moment with anatarajia kufanya kipindi na msanii wa filam JACKSON KABIRIGI.

"Lengo langu ni kukonga nyoyo za watu kwa kuwatimizia kila ambacho wanakihitaji kutaka katika kipindi cha a moment with kwa sasa nipo katika maandalizi ya kipindi hicho na nimekuwa nikipokea maoni mbali hasa kwa watu ambao nimekuwa nikiwashirikisha juu ya idea ya kipindi cha a moment with ambacho natarajia kianze kuwa hewani hivi karibuni katika moja ya vituo vikubwa vya television hapa Tanzania watu wengi wameonyesha kukikubali na kuomba japo kwa kipindi cha mwanzoni nimwalike JACKSON KABIRIGI kwani wamekuwa wakitamani kujua mengi sana juu yake" alisema Eid Palmer ambaye ndiye mtangazaji wa kipindi hicho cha A moment with ambacho anakifanya akiwa ndani ya kampuni za MAGIC SCREEN na TIMAMU EFFECTS.

RED & GREEN MOVIE IS COMING SOON

filamu mpya ya kitanzania iliyorekodiwa kwa kiwango cha kimataifa chini ya kampuni mbili zilizobobea katika utengenezaji wa filam nchini Tanzania MAGIC SCREEN na TIMAMU EFFECTS, inatarajiwa kuingia sokoni mapema mwaka 2011, kwa sasa ipo jikoni ikifanyiwa editing na maujanja ya kimataifa.
filamu hiyo ambayo imekutanisha wasanii pamoja na watendaji wa production wenye uwezo wa hali ya juu katika kazi, kwa upande wa wasanii ambao wameshiriki ni pamoja na JACKSON KABIRIGI aliyewahi kutamba katika filamu kama born to suffer, nunda, cross roads, my nephew na nyingine nyingi, pia yumo DENIS DAVID aliyewahi kung'aa katika fulamu ya Temtation na nyingine nyingi, pia wamo wasanii kama baga, mohamed ( M2 ), Bi mariam, Annie pamoja na wengineo wengi. pia kwa upande wa production crew wamesimama HANS HIDA na TIMOTH CONRAD katika upande wa kupiga picha na editing, pia DIRECTOR wa filamu hiyo ni TIMOTH CONRAD wakati HANS HIDA amesimama katika kitengo cha DIRECTOR OF PHOTOGRAPH, pia BARAKA amesimama kama CRANE OPARETOR.
ki ukweli filamu hiyo imetulia sana na inatarajiwa kuziteka nyoyo za watazamaji....
tembelea www.timamu.webs.com ili kupata habari zaidi juu ya RED & GREEN
KAENI MKAO WA KULA