TICO EDITOR

Wednesday, January 5, 2011

TINO MWIZI - PRODUCER AKIM

Muandaaji wa filam nchi Tanzania Akim Natibu maarufu kama Akim Producer, aliyewahi kuandaa filam ya damalisa, ameieleza Timamu Habari juu ya kitendo cha kihuni alichofanyiwa na Msanii wa filam nchini Tanzania Hisani Hassan Muya maarufu kama Tino.

"mwanzoni nilimwamini sana na nilitamani kumpashavu ili awe mmoja kati ya washiriki katika filam yangu mpya ninayoiandaa hivi sasa, hivyo tukafikia makubaliano ya bei na akahitaji nimlipe advance (kianzio) ili itakapofika siku ya kuanza kazi ya kurekodi filamu hiyo nimalizie kiasi kilichobakia, lakini cha kushangaza siku mbili kabla ya kazi kuanza nilimpigia simu ili kumkumbusha juu ya kazi hiyo alinambia kuwa yupo zanzibar kikazi na siku hiyo itakapofika atakuwa amesharudi hivyo ataweza kufika location" alisema Akim Producer

pia aliendelea kusema kuwa chakushangaza ilipofika siku ya kazi Tino hakutokea location na alipopigiwa simu hakupokea hivyo ikabidi achukuliwe mtu mwingine ili awezekukava nafasi yake, lakini baada ya siku mbili tangu kazi ianze akim alimpigia tena simu na safari hii alipokea na kusema kuwa bado hajarudi na siku atakaporudi atarudisha pesa aliyopewa kama advance kwani kazi yenyewe hakuifanya.

"lakini chakushangaza nimepata habari kuwa tayari amekwisharudi na yupo hapa dar na nikimpigia simu ili nionane nae anipatie hela yangu amekuwa hapokei simu yangu" alisema akim kwa uchungu wakuibiwa pesa zake.

kadhalka pamoja na kumdhulumu pesa pia akim amesema kuwa amemdhulumu pia jina la filamu hiyo ( HARD TIME ).

"wakati namkabidhi script ya filam yangu ya hard time tino aliwahi kuniambia kuwa anataka nimuuzie jina hilo kwani amelipenda lakini sikumkubalia matokeo yake hivi juzi niliona tangazo la filam mpya ambayo yeye tino pia ameshiriki ikiwa inaitwa HARD TIME kama jinsi jina la filam yangu ilivyo" alisema akim

"kwakeli Bado sijamsamehe Tino kwakitendo alichokifanya ila ninachokitaka anilipe pesa zangu na kuhusu swala la jina la filam sina wasi wasi kwani ninajiamini kuwa ninauwezo mkubwa katika utunzi wa filam hivyo nitaweza kupata jina lingine" alisema akim

Timamu Habari baada ya kupata habari hizo ilimtafuta Tinno ili kumuuliza juu ya tuhuma hizo bila mafanikio kwani hakupokea simu... lakini tunachoweza kukisema kama maneno ya Akim Producer niyakweli basi Tino inampasa arudishe pesa za watu ili asijichafulie jina na si vizuri kufanya kitendo kama hicho.