DOCTOR SLAA APATA KIPIGO AKIWA KATIKA MAANDAMANO YA AMANI JIJINI ARUSHA
MABOMU, RISASI, VIPIGO na hatua ya Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana vilisababisha amani kuvunjika na damu kumwagika katika mitaa ya jiji la Arusha wakati jeshi hilo likijaribu kuwasambaratisha maelfu ya wafuasi waliokuwa katika maandamano ya amani.