TICO EDITOR

Thursday, January 6, 2011

MIMI NA JACK KWA SASA SIO WAPENZI - SABRINA

hivi karibuni kulikua na uvumi juu ya uhusiano baina ya wasanii wawili wafilam walioshiriki katik filam ya cross roads, Jackson Kabirigi a.k. Nunda na Sabrina.
Habari zilizotufikia kutoka kwa chanzo chetu cha habari zilisema kuwa wasanii hao wawili wamekuwa wakionekana katika kumbi mbalimbali wakiwa pamoja katika mikao isiyoeleweka ( '0' distance ) chanzo chetu cha habali kilipeleleza na kupata kuzungumza na rafiki wa karibu wa jackson ambaye hakupenda jina lake liandikwe alisema
"kwakeli jack aliwahi kuniambia kuwa kuna mmoja kati ya wasanii alioshiriki nao katika filam yake mpya ya cross road kuwa "anakula mzigo" lakini hakuwahi kuniambia ni nani, hivyo hata mimi nashangazwa nakitendo cha yeye kuwa karibu sana na sabrina mi nahisi kuna kitu kinaendelea between them"

Timamu habari haikuchoka ikamtafuta jack mwenyewe ili aeleze ukweli juu ya hili lakini hakuweza kutoa ushirikiano wakutosha juu ya hilo
"siko tayari kulizungumzia hilo swala kwa sasa labda uniulize ninatarajia kutoa filam gani kwa sasa na sio huo u***" alimalizia jackson na kukata simu

Pamoja na hayo hatukukata tamaa tukatia maguu mpaka nyumbani kwa sabrina
"si mara ya kwanza kuulizwa swali hilo na sijui ni kwanini watu wanapenda kufatilia mambo ya watu, ki ukweli kabisa mimi na jack hatuna uhusiano wa kimapenzi bali ni marafiki tu nawashangaa wanaodhani mimi na jack ni wapenzi" alisema sabrina kwa msisitizo pia alipoulizwa kuwa kwa sasa anatoka na nani alisema "ninae mtu ninaempenda kwa sasa lakini siko tayari kumuweka wazi ila muda utakapofika nitaweka wazi kila kitu" alimalizia sabrina.