TICO EDITOR

Thursday, January 6, 2011

LETHAL POISON INAZIDI KUFANYA VIZURI SOKONI

filam ya lethal poison ambayo imeingia sokoni wiki moja iliyopita, inaendelea kufanya vizuri kimauzo.

"Licha ya kwamba tumepata hasara sana katika utengenezaji wa filamu hiyo, kwa sasa nafarijika kwani watanzania wameonyesha kuikubali na kuipokea kwa mikono yote miwili naamini kama wakiendelea kuinunua kwa kasi kama ilivyokuwa kwa wiki hii ya kwanza nitafarijika zaidi" alisema Jairos kachota ambaye ndiye 'producer' wa filamu hiyo.

ndani ya filam hiyo iliyorekodiwa mkoani mbeya pia ameshiriki gwiji wa filam za kitanzania steven kanumba pamoja na wasanii wengine wa mkoani mbeya akiwemo Dennis Louis, Thomas na wengine wengi.

"Filam ya lethal poison ni nzuri na kilichonifurahisha zaidi editing iliyofanyika imeifanya filamu hiyo iwe nzuri zaidi" alisema Steven Kanumba.
cameraman aliyepiga picha filamu hiyo ni Timoth conrad 'TICO' vile vile yeye ndeye aliyeifanyia editing akiwa katika kampuni ya TIMAMU EFFECTS.