TICO EDITOR

Thursday, May 19, 2011

HATUA YA KIMATAIFA

Ni baada ya ukimya wa muda mrefu sasa Jackson Kabirigi aka mzee wa hisia ukipenda unaweza kumuita Nunda ambae ni director,akiwa pamoja na Denis David ama wengi wamemzoeya kama mzee wa Tampetion wakiwa katika picha ya pamoja ambayo inautambulisha ujio wao mpya kabisa katika filamu ya HOME VILLAGE ambayo ipo karibuni kuingia sokoni ikiwa imewakutanisha wasanii mbalimbali wa nje na ndani ya tanzania.Kama vile msanii Dady Ramadhani kutoka South Africa ambaye ametamba katika filamu ya MY NEPHEW MONEY TRANSFER ambaye amefanya vizuri katika HOME VILLAGE.vilevile katika filamu ya HOME VILLAGE utakutana na wasanii wengine wa hapa nchini kama vile Omari Clayton ambaye kwa sasa anatamba na filamu ya HEKIMA,Latifa Idabu,Sabrina Omary na wengine wengi,filamu ya HOME VILLAGE ni filamu ambayo imefanywa katika ubora wa kimataifa na inatarajiwa kureta mapinduzi makubwa katika soko la filamu ndani na nje ya Tanzania,msemaji mkuu wa kampuni ya TIMAMU EFFECTS ambayo ndio imeiandaa filamu hiyo bw.Timoth Conrad ambae pia ndio camera man na editor wa filamu hiyo amesema kuwa watanzania watarajie kupata kitu ambacho kitawaonyesha kuwa sasa kweli Tanzania kuna waandaaji wa filamu zenye ubora wa kimataifa,kazi kwako wewe mdau na mpenzi wa filamu Tanzania.