077 Day’s imetayarishwa na kampuni ya Wajey Film Company ikishirikiana na Timamu Effects zote za jijini Dar es Salaam, filamu hiyo inaongelea mambo ya miujiza ambayo yaliwahi kutokea miaka ya nyuma, ni filamu ambayo inatarajiwa kuwa ya aina yake kwa sababu ya mfumo wa hadithi ulivyotumika na wasanii jinsi walivyocheza kwa hisia huku ikiwa imerekodiwa nje ya jiji la Dar es Salaam, akiongea na FC Sajuki alisema.
“Filamu hii nategemea ilete mapinduzi makubwa kabisa katika tasnia hii ya filamu na wapenzi wangu wenyewe wanajua uwezo wetu katika sanaa, na mfano mliuona katika filamu iliyopita na kufanya vizuri sana ya Vita Mkomanae hadi kuweza kuchukua tuzo kwa mwaka huu, tuzo hii kwetu sisi Wajey Film Company imekuwa chachu ya kufanya kazi kwa nguvu”
Alimalizia kwa kuongea Sajuki ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni hiyo.
Filamu hii imeandikwa na Timoth Conrad na kuongozwa na Juma Kilowoko (Sajuki) akishirikiana na Timothy Condard (Tico), wasanii walioshiriki ni Nassoro Ndambwe ( Zigamba) Wastara Juma , Juma Kilowoko na wasanii wengine nyota na wakali, filamu hiyo ipo studio katika hatua za mwisho katika uhariri, na inatarajia kutoka hivi karibuni.