TICO EDITOR

Thursday, December 23, 2010

SIKUWAHI KUOTA KUWA MUIGIZAJI - JACKSON KABIRIGI

JACKSON KABIRIGI aushangaza umati wa watu baada ya kutoa historia yake katika mtandao unafuatilia habari za wasanii wa Tanzania na kuziweka hewani (http://timamu.webs.com)pale aliposema kuwa hakuwahi kuota kuwa muigizaji bali ndoto zake zilikuwa ni kuwa msanii wa kuimba hasa muziki wa bongo fleva na ragaton.

JACK aliyewahi kutamba katika filam za Born to suffer, Nunda, My nephew, Cross Roads ameiambia Timamu effects habari kuwa katika maisha yake amekuwa akiwaza kuja kuwa msanii wakuigiza tofauti na watu wanavyodhani kuwa yeye alikuwa na ndoto za kuwa msanii wakuigiza ndio maana anafanya vizuri katika kila kazi anayopea kushiriki.

"kipindi naingia dar nilikuja kwa lengo moja tu kupeleka nyimbo zangu redioni na kuzipromot kisha kuanza kusambaza albamu yangu niliyoirekodia nchini uganda, lakini sikufanikiwa hata kidogo hivyo nikaambulia kujiingiza katika sanaa ya uigizaji" alisema Jackson katika waraka wa histori ya maisha yake aliouanika katika mtandao wa timamu effects news...

TIMOTH CONRAD ' TICO ' THE BEST CAMERAMAN & FILM EDITOR

JACKSON KABIRIGI NI ZAIDI YA ACTOR - AKIM

Muandaaji wa filamu za kitanzania aliyewahi kuandaa filamu ya damalisa iliyowahi kutamba kunakosoko la filamu nchini Akim Natibu Igembe, ameweka wazi kuwa hajawahi kukutana na muigizaji mwenye kipaji kama alichonacho jackson kabirigi aliyewahi kutamba katika filamu za MY NEPHEW, CROSS ROADS, NUNDA, BORN TO SUFFER,

"kwakweli licha ya kwamba jackson ni rafiki yangu lakini lakini pia ndiye mtu ninaeamini anaweza kufanya kila kitu ambacho atahitajika kukifanya katika kazi ya kuigiza" alisema Akim alipokuwa akizungumza na timamu effects news wakati wakiwa location wakiendela na shooting ya filamu mpya itakayokwenda kwa jina la HARD TIME.

FILAMU YA BRIEFCASE IMEINGIZWA KATIKA TUZO ZA MIN ZIFF

Filamu mpya ya briefcase iliyotengenezwa na kampuni ya WAJEY FILM ikishirikiana na TIMAMU EFFECTS zote za dar. imeonyesha record nzuri kimauzo tangu ilipoingia kunoko soko la filam nchini.
kutokana na ubora wa filamu hiyo yakitanzania iliyotengenezwa katika kisiwa cha zanzibar waandaaji wa tuzo za MIN ZIFF wameamua kuipendekeza ingiie katika kinyanganyiro cha kugombia tuzo ya filamu bora.
"Kwakweli najisikia vizuri sana kuona jinsi watu wanavyokubali na kuzipenda kazi zetu na mpaka kufikia hatua yakuipendekeza kuingia katika MIN ZIFF, na ninaimani itafanikiwa kuchukua tuzo hizo kutokana na ubora wafilamu yenyewe" alisema Wastara juma ambaye ndiye mtunzi wa filamu hiyo.
"mimi binafsi nilipopata habari ya filam yetu ya briefcase kuingia katika tuzo sikushtuka sana kwani nilikuwa namatarajio hayo, ila nilifurahi na kuishukuru sana crew ambayo nimekuwa nikifanya nayo kazi zetu pia namshukuru zaidi TIMOTH CONRAD ' TICO ' ambaye ndiye editor wa filam hiyo kwa uwezo wake mkubwa waubunifu kwani amechangia kwa kiasi kikubwa kuiboresha filamu hiyo..." alisema Juma kilowoko 'sajuki' alipokuwa akizungumza na Timamu effects news.
kupata habari zaidi juu ya filamu hiyo tafadhali tembelea www.timamu.webs.com

TIMOTH CONRAD ' TICO ' KAZINI

Wednesday, December 15, 2010

NIMEOKOKA KIKWELI JAPO WATU HAWANIAMINI - Mainda

hivi karibuni Mainda a.k.a Binti mlokole ameweka wazi kukerwa kwake na kitendo cha baadhi ya mashabiki wake kumkejeli kwamba hawezi kuokoka na kudai kuwa amezidi umachepele...

"Mimi sio machepele na kusema kweli nakerwa sana na kitendo cha baadhi ya watu kunibeza kwa kitendo changu cha kutangaza kwamba nimeokoka, sijui kwa nini watu hawaniamini?" alisema Mainda alipokuwa akizungumza na Timamu Effects ndani ya viwanja vya Ledaz jijini dar.

QUEEN OF BONGO FILM KUFANYA BONGE LA SHOO SIKU YA CHRISMAS

Tarehe 25 mwezi wa 12 ndani ya jiji la mwanza kutakuwa na tukio lakihistoria ambapo quen of bongo film (WASTARA JUMA) akiambatana na wasanii kama Juma kilowoko, Z. Anton, H. baba, Zigamba pamoja na wasanii wengine wengi watatoa burudani kwa mashabiki wa jijini Mwanza ndani ya VIWANJA VYA CCM KIRUMBA...
"lengo lakufanya shoo hii ni kutaka kutoa burudani kwa mashabiki wetu, sababu tumegundua kuwa wapo wadau wetu wengi ndani ya jiji la mwanza na wanatamani japo siku moja wakutane na sisi ana kwa ana na kupata burudani LIVE" alisema Queen of bongo film (wastara Juma), pia Juma kilowoko ambaye pia atakuwepo na kutoa sapoti kubwa katika shoo hiyo inayotarajiwa kukata kiu ya burudani ya wakazi wa mwanza alisema kuwa huu ni mwanzo na kwamba mara watakapo maliza shoo hiyo jijini mwanza wanatarajia kuzunguka baadhi ya mikoa mingine ya hapa nchini ili pia kukonga nyoyo za mashabiki.
ndani ya shoo hiyo pia kutakuwa na burudani tofauti tofauti zikiwemo ngoma za asili kutoka kwa Zigamba akiwa na kundi lake, pia itashereheshwa na Z. Anton mzee wa kisiwa cha malavidavi, pamoja na H. Baba.
"kiukweli tunaisubiri kwa hamu kubwa shoo hiyo kwani tumekuwa tukitamani japo siku moja tuwaone sajuki na wastara kwa kweli tumekuwa tukinunua sana kazi zao na tunazipenda sana kwakweli" alisema shabiki mmoja wa burudani jijini mwanza...

TIMAMU EFFECTS INAWATAKIA BURUDANI NJEMA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA

Saturday, December 11, 2010

NIPO CHIMBO NAIUNDA VOLCANO - DENIS WA TEMPTATION

Denis Devid aliyewahi kung'ara katika filamu ya TEMPTATION aeleza wazi jinsi anavyoiunda volcano na kufafanua kuwa hana lengo la kuiangamiza dunia kwa volcano anayoitengeneza bali analengo lakuitetemesha tasnia ya filamu nchini baada ya kukaa kimya tangu alipotoka na filamu ya TEMPTATION.
"Kwakipindi kirefu nimekuwa kimya lakini nataka kuwaambia wadu kuwa nilikuwa chimbo nikipata mafunzo ya jinsi ya kuiunda volcano ambayo naamini itaitikisa tasnia ya filamu na kuwafanya wadau kuamini kuwa nililetwa duniani kwa lengo lakuushangaza ulimwengu" alisema Denis alipokuwa akiongea na TIMAMU EFFECTS.
Pia alipoulizwa ni ujio gani anatarajia kuja nao baada ya TEMTATION akasema kuwa "wadau watarajie vumbi katika FANS TOUR filamu mpya iliyotengenezwa kwa kiwango cha kimataifa chini ya kampuni ya MAGIC SCREEN iliyopo jijini Dar"

SAJUKI NA STARA KUJA NA 077 DAYS

Juma Kilowoko na Wastara Juma

Sajuki na Stara

BAADA ya muda mrefu kutamba na filamu zenye majina ya lugha adimu ya Kiswahili hatimaye muigizaji na muongozaji mahiri wa filamu hapa Tanzania Juma Kilowoko maarufu kama Sajuki amejikuta akiingia katika mtego wa kuanza kutumia majina ya kigeni, hivi karibuni amefanikiwa kurekodi filamu inayokwenda kwa jina la 077 Day’s, filamu hii imerekodiwa Wilayani Songea Mkoani Ruvuma.

077 Day’s imetayarishwa na kampuni ya Wajey Film Company ikishirikiana na Timamu Effects zote za jijini Dar es Salaam, filamu hiyo inaongelea mambo ya miujiza ambayo yaliwahi kutokea miaka ya nyuma, ni filamu ambayo inatarajiwa kuwa ya aina yake kwa sababu ya mfumo wa hadithi ulivyotumika na wasanii jinsi walivyocheza kwa hisia huku ikiwa imerekodiwa nje ya jiji la Dar es Salaam, akiongea na FC Sajuki alisema.

“Filamu hii nategemea ilete mapinduzi makubwa kabisa katika tasnia hii ya filamu na wapenzi wangu wenyewe wanajua uwezo wetu katika sanaa, na mfano mliuona katika filamu iliyopita na kufanya vizuri sana ya Vita Mkomanae hadi kuweza kuchukua tuzo kwa mwaka huu, tuzo hii kwetu sisi Wajey Film Company imekuwa chachu ya kufanya kazi kwa nguvu”
Alimalizia kwa kuongea Sajuki ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni hiyo.

Filamu hii imeandikwa na Timoth Conrad na kuongozwa na Juma Kilowoko (Sajuki) akishirikiana na Timothy Condard (Tico), wasanii walioshiriki ni Nassoro Ndambwe ( Zigamba) Wastara Juma , Juma Kilowoko na wasanii wengine nyota na wakali, filamu hiyo ipo studio katika hatua za mwisho katika uhariri, na inatarajia kutoka hivi karibuni.

Friday, December 10, 2010

JACKSON KABIRIGI APANIA KUFANYA MAKAMUZI KATIKA RUGS BEGINNING...

Jackson kabirigi aliyewahi kutamba katika filam za Born to suffer, Nunda, My Nephew, Cross Road iliyotoka hivi karibuni apania kufanya makamuzi yakufamtu ndani ya filam mpya inayoandaliwa chini ya kampuni za TIMAMU EFFECTS na MAGIC SCREEN...

"japokuwa watu wamekuwa wakinikubali hasa kutokana na uwezo wakiuchezaji ambao nimekuwa nikiuonyesha katika baadhi ya filam ambazo nimewahi kushiriki, kwa sasa nataka kuwaonyesha zaidi watanzania na watu wengine Africa na dunia nzima kuwa nilizaliwa kuja kuushangaza ulimwengu" alisema jackson kabirigi

pia aliongeza kuwa ndani ya film hiyo ambayo nayeye pia ni mmoja kati ya jupo la watunzi wa filam hiyo itakuja kuwashitua watazamaji ambao wamekuwa wakidhani kuwa 'wazungu' pekee ndio wanaweza kutengeneza movie ambayo itamfanya mtazamani asinyanyuke mara anapoanza kuitaza.

"sihitaji kuongea mengi sana ila waingoje kazi kwa hamu" alisema jackson kwa kujiamini...

TUMEFUNGUA BLOG MPYA www.timamu.webs.com

Tumefungua blog yetu mpya ambayo itakuwa ikikuonyesha kazi zote ambazo zinafanywa na TIMAMU EFFECTS PRODUCTION...
bonyeza hapa kutembelea blog yetu mpya www.timamu.webs.com
'ENJOY YOUR SELF'

Monday, December 6, 2010

077 DAYS is Coming soon...

filam mpya itakayoitwa 077 DAYS iliyotengenezwa kwa kiwango cha kimataifa kwa ushirikiano mkubwa wa kampuni mbili, moja ikiwa ni TIMAMU EFFECTS na WAJEY FILM CO. inatarajiwa kuingia sokoni mapema mwakani na kutarajiwa kufunika kimauzo katika soko la filamu nchini.
pia filamu hiyo imeshirikisha wasanii wenye uwezo na kazi zao kama Juma kilowoko (sajuki), Wastara Juma, Nassoro Ndambwe, Zigamba na wengine wengi...
hii ni crew iliyoshiriki kuikamilisha filam hiyo

Story: Timoth Conrad, Wastara juma
Camera/editing: Timoth conrad (Tico)
location manager: Nassor Ndambwe
Make up & costume: Wastara juma
visual effects: Timoth conrad (Tico)
Director: Juma kilowoko (sajuki)
Asst. Director: Timoth Conrad (Tico)

click here to watch 077 trailer>>

Sunday, October 17, 2010

FILAMU MPYA YA CROSS ROAD IKO NJIANI

Watanzania kaeni mkao wa kula CROSS ROAD filam bora ya kitanzania iko njiani muda si mrefu itaingia kunako soko...
filamu hiyo imewashirikisha wasanii wenye uwezo kama Hemed Suleiman, Jackson Kabirigi, Glady, Badra na wengineo wengi...

Sunday, September 26, 2010

JACKSON KABIRIGI NA TIMOTH CONRAD

I'M A FIGHTER NI ZAIDI YA MY NEPHEW - JACKSON KABIRIGI



Jackson kabirigi aweka wazi kuwa filamu mpya anayoitengeneza kwa hivi sasa akiwa ndani ya kampuni ya TIMAMU EFFECTS ambayo ameipa jina la I'M A FIGHTER itakuja kufunika ile mbaya soko la filamu nchini.
akiielezea kwa ufupi filamu hiyo alisema ni filamu imbayo imegusa hisia zote hivyo kulingana na uwezo aliouonyesha ndani ya filamu hiyo anaamini kuwa ni zaidi ya kiwango alichokionyesha ndani ya filamu ambay iliwahi kutikisa vilivyo kunako market ya filamu zakibongo MY NEPHEW ilichezwa nchini Africa ya kusini na hapa nyumbani Mbeya Tanzania...

Friday, September 24, 2010

BONGO MOVIE MISTAKES

Timamu Effects imeanzisha kurasa ambayo itakuwa ikikuonyesha makosa ambayo yamekuwa yakifanyika katika baadhi ya filamu zetu zakitanzania (BONGO MOVIE MISTAKES), ndani ya page hiyo utapata kuona baadhi ya filamu zakitanzania ambazo zinamakosa ya wazi kabisa na yandani ambayo yamejificha...
Bonyeza hapa kuona filamu gani tumeichambua kwa wiki hii na makosa yake

Monday, September 20, 2010

BAADA YA DAMALISA SASA NI HIDEN TRUTH

Baada ya filamu ya DAMALISA kuingia sokoni na kupokelewa vizuri na mashabiki wa filamu za kutisha, sasa AKIM NATIBU ambaye ndiye aliyeiproduce filam hiyo ya DAMALISA, anaandaa filamu nyingine ambayo anatarajia itakuwa bomba kuliko DAMALISA.

Pia filamu hiyo ambayo ameipa jina la HARD TIME (Ukweli uliofichika), inatarajia kuanza kurekodiwa mara ifikapo mwezi 11 mwaka huu, "ni matarajio yangu kuwa mashabiki wataipokea kwa mikono yote miwili, na pia wataifurahia kwani ni story inayoelezea maisha halisi ya Mtanzania" alisema Akim ambaye ni manager pia wa MASTER ARTS GROUP.

Filamu hiyo yenye matukio ya kusisimua inataraiwa kurekodiwa na TIMAMU EFFECTS kampuni ambayo ilitengeneza pia filamu ya DAMALISA, Akim alipoulizwa ni kwanini asifanye na kampuni nyingine tofauti na TIMAMU EFFECTS, alisema kuwa imani yake inamuonyeshakuwa bado hajapata kuona kampuni ya utengenezaji wafilamu ambayo itakidhi mahitaji yake kuanzia Quality ya picha mpaka editing...

JUMA KILOWOKO SAJUKI AOKOA MAISHA YA MKEWE WASTARA

Hivi karibuni kumeibuka habari juu ya simu za maajabu ambazo zinasemekana kuleta madhara makubwa sana hapa Tanzania, awali mratibu wa mawasiliano nchini aliripoti kuwa hakuna uthibitisho wa aina yoyote juu ya swala hili na hivyo kumaanisha kwamba hakuna madhara ya aina yoyote katika matumizi ya vyombo vya mawasiliano hususani simu za mkononi, hivyo habari zinazoenezwa na baadhi ya watu kuhusu kutokea kwa madhara mara tu mtu anapopigiwa simu kwa namba ambazo hazieleweki mfano. 0000000000000000, mara tu anapopokea hupoteza maisha ama kupararaizi ni uzushi mtupu.

Katika hali isiyo ya kawaida hivi karibuni msanii wa maigizo Wastara Juma aliyewahi kutamba na filamu ya Mboni yangu, 2Brothers, Round, Vita Mkomanae, alipigiwa simu na moja kati ya namba hizo ambazo hazieleweki hivyo alimtaarifu mumewe Juma Kilowoko juu ya simu hiyo. ndipo mumewe alipokurupuka na kumpokonya simu mkewe na kumkataza asije akaipokea kwani anaweza kupoteza maisha au kupararaizi
Ingawa Wastara hakuonesha kuamini maneno hayo na kudai kuwa alitarajia kupokea simu kutoka nje ya nchi hivyo mara nyingi simu za kutoka nje huwa hazionyeshi namba ya mpigaji bali huwa inaonekana 'private no' or 'unknown call' hivyo kusababisha mabishano baina ya wapendanao hao wawili na mwisho kufikia muafaka wa kutoipokea simu hiyo...

JACKSON KABIRIGI WA TANZANIA AFANANISHWA NA CHWENEYEGAYE (TSOTS) WA SOUTH AFRICA


Msanii wa filamu nchini Tanzania Jackson Kabirigi, aliyewahi kutamba katika filamu ya BORN TO SUFFER, MY NEPHEW, NUNDA na nyinginezo, hivi karibuni alijikuta akipigwa na butwaa baada ya baadhi ya mashabiki wake waliopo nchini Afica ya Kusini kumpachika jina la TSOTS wa BONGO,

"kiukweli nilishangaa sana na nilipochunguza kwanini wananifananisha na msanii huyo ambaye makazi yake ni nchini Africa ya Kusini, baadhi ya watu waliniambia kuwa kufananishwa kwangu kulitokana na jinsi nilivyoigiza katika filamu ya MY NEPHEW iliyofanywa nchini South Africa" alisema Jackson kabirigi.

Ndani ya filamu hiyo iliyorekodiwa na kuongozwa na RASHID MRUTU, pia kufanyiwa editing na TIMOTH CONRAD wa TIMAMU EFFECTS, wameshiriki waigizaji wakubwa kutoka nchini Africa Kusini, Botswana, Ghana, Uganda, Tanzania...